Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Baraka Kizuguto (pichani) kuwa Ofisa Habari kuanzia Februari 1 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Kizuguto alikuwa Ofisa Habari wa klabu ya Young Africans, nafasi aliyoitumikia kwa miaka miwili.
Kizuguto
ana Stashahada ya Juu ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha LEARN IT
cha Dar es Salaam. Pia ana ujuzi wa kusanifu tovuti, ufundi wa kompyuta
na uchambuzi wa mifumo ya kompyuta.
Mei
mwaka jana, Kizuguto aliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) kuhudhuria mafunzo ya usajili na uhamisho wa kimataifa wa
wachezaji kwa njia ya mtandao (TMS) yaliyofanyika Johannesburg, Afrika
Kusini.
TFF inamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.