Kiungo wa timu ya Simba SC Christopher Alex Masawe Afariki Dunia

Aliyekuwa kiungo wa timu ya Simba SC Christopher Alex Masawe amefariki dunia jana saa 3 Asubuhi katika hospitali ya Milembe mkoani Dodoma baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa mama yake mzazi aliyekuwa akimuuguza, maziko yatafanyika keshokutwa siku ya Jumanne.

Christopher Alex atakumbukwa kwa kufunga penati ya mwisho katika mchezo wa Simba dhidi ya Zamalek na kuifanya Simba ifuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika mwaka 2003 mchezo uliopigwa nchini Misri.

Baadhi ya wachezaji waliounda kikosi hicho kilichoitoa Zamalek ni pamoja na Boniface Pawasa, Juma Kaseja na Suleiman Matola.

Rais wa Simba Evans Aveva ambaye yuko mjini Shinyanga katika pambano la ligi kuu dhidi ya Stand United ametuma salam za rambirambi kwa familia ya marehemu na kumuelezea marehemu kuwa aliitumikia Simba kwa juhudi, mapenzi na uaminifu mkubwa na kusema kwamba Simba itaungana na familia yake katika msiba huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo