Meneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Mpekuzi, Babu Tale alisema watakuwa wehu
kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili
kupata fedha, lakini ukweli ni kwamba hawajapewa kitu chochote.
Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote
atakayetangazwa kuiwakilisha CCM.
“Kama kweli tungekataa fedha hizo hata
Mwenyezi Mungu angetulaani, ila naamini taarifa hizo zitakuwa
zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kumchafua, hajawahi kutupa
ofa hiyo,” alisema Babu Tale.