Zaidi ya wanafunzi 600,000 wahofu kutopiga kura uchaguzi mkuu ujao

Zaidi ya wanafunzi laki sita wa vyuo vikuu, vyuo vya kati na kidato cha nne nchini huwenda wasishiriki kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao kutokana na ratiba ya wizara ya elimu kuhusu mihula ya kufunga na kufungua vyuo nchini kukinzana ya NEC.

Ratiba ya mihula ya kufunga na kufungua vyuo ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu mwaka huu, imeibua hofu kwa wasomi wa vyuo mbalimbali nchini kutoshiriki ipasavyo kwenye uchaguzi mkuu ujao, ambapo jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO) mkoani Mbeya wamelibaini hilo na kuanza kupaza sauti zao kuidai haki hiyo.
 
Kutokana na hofu hiyo, CHASO imeandika waraka na kuuelekeza katika ofisi ya katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo ikimtaka kuwatumia wabunge wake kupeleka hoja binafsi bungeni ya kurekebisha sheria ya uchaguzi ili iwaruhusu watanzania wote kupiga kura wakiwa mahali popote ndani ya mipaka ya Tanzania.
 
Baadhi ya wanafunzi hao pia wameelezea umuhimu wa wao kupiga kura, huku wakidai kuwa hawako tayari kunyimwa haki yao ya kikatiba kwenye uchaguzi mkuu ujao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo