Watu
zaidi ya 8 wamenusurika kifo wakati wakiwa wamelala nyumbani mwao mtaa
wa heri manispaa ya tabora, baada ya gari la mizigo aina ISUZU
kuparamia nyumba yao, lilipomshinda dereva alipokuwa akikata kona,
ambapo mama mjazito aliyenusurika amekimbizwa hospitalini akiwa na hali
mbaya kutokan a na mshituko na hali yake ya ujauzito.
Wananchi na mashuhuda wa ajali hiyo
walioharibiwa thamani zao mbali mbali wamesema kuwa, umefika wakati
serikali kubadili adhabu za madreva wazembe ambao wanaendesha vyombo vya
usafiri bila kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali huku wakipoteza
maisha ya wananchi na mali zao.
Akizungumza juu ya ajali hiyo na kubaini uzembe wa dereva
wa gari hilo lenye namba za usajili t 396 AGS, ambaye hakupatikana mara
moja, kamanda wa polisi mkoani tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda
aliyefika eneo la ajali hiyo amesema kuwa, mwendesha gari hilo
atatafutwa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha mmiliki wa nyumba hiyo bw.Ramadhani Musa Kaswezi, anayeishi
kijijini ilolangulu hakusema lolote akidai kikao cha familia kitatoa
maamuzi ili kuelezea hatua atakazochukua kutokana na wapangaji wake
wawili kubolewa nyumba.