Tumesikia kuhusu ajali nyingi za Bodaboda, hivi unajua ni hasara kiasi gani imetokana na ajali hizo? majibu yapo hapa

ajali 4Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za pikipiki na kugharimu maisha ya watumiaji wa usafiri huo tangu Serikali ilipoidhinisha matumizi ya vyombo hivyo mwaka 2009.

Waziri Mwakyembe amesema ongezeko hilo limesababisha hasara ya shilingi trilioni tatu kutokana na matibabu kwa majeruhi na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
DSC07217… Kutokana na ajali hizo inakadiriwa kwamba Taifa limepoteza zaidi ya shilingi trilioni 3.2 mwaka jana tuu… kwa maana ya uharibifu wa vyombo vingine vya usafiri, uharibifu ya miundombinu , gharaza za matibabu na bima, gharama za uokoaji na usimamizi, upotevu na uharibifu wa mali kwenye magari husika na Sumatra nawaombeni sana hebu washirikisheni wenzenu trafiki wale… Kamanda Mpinga anzisheni jamani uhusiano wa karibu na waendesha pikipiki kupitia asasi yao hii sasa ya mafunzo hii ya APEC… Hebu kuweni karibu sana... ”Waziri Mwakyembe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo