Moja kati ya story zilizoshtua wapenda michezo nchini England mwishoni mwa wiki hii ni ajali ambayo aliipata nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England David Beckham .
Becks alipata mkasa huo wakati akiwa anatoka kumchukua mwanae anayefahamika kwa jina la Brooklyn toka kwenye mazoezi ya kila siku ya timu yake ya Arsenal .
Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita .
Picha inayoonyesha magari mawili likiwemo la David Beckham lililopo upande wa kulia baada ya ajali aliyoipata star huyo.
Picha inayoonyesha familia nzima ya Beckham akiwa na mkewe Victoria Beckham na wanae wa kiume Brooklyn , Romeo na Cruz.