PROFESA KAPUYA AMNUSURU DR.MWAKYEMBE HUKO KYELA

  Na Ibrahim Yassin,Kyela   

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Juma Kapuya amemnusuru mbunge wa jimbo la Kyela na waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe (CCM) alipozuiwa na wananchi wa jimbo hilo wakitaka atoe maelezo ya kushindwa kuziondoa changamoto za muda mrefu zilizopo wilayani humo.   

Dr. Mwakyembe alikutwa na kadhia hiyo jana wakati kamati hiyo ilipokuwa ikifanya ziara ya kukagua miradi ya miundombinu ikiwemo barabara kuu ambayo imekuwa ikijengwa chini ya kiwango kila mara ambapo wakiwa katika msafara wakielekea Bandari ya Itungi wananchi walizuia msafara huo.   

Baada ya kuzui msafara huo wananchi walimuuliza maswali mbunge huyo kuwa Kyela imekuwa haina maendeleo huku yeye akihamia Dar es salaam na kushindwa kuwajibika kama alivyoahidi kufanya hivyo wakati akiomba kura za ubunge mwaka 2005 ambapo amewageuka alipopata ubunge.   

Elieza Mwankemwa mkazi wa Kyela mjini alimuuliza mbunge huyo kuwa barabara kuu haijawahi kuwa na ubora tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961 na imekuwa ikibomolewa na kuwekwa viraka kila mwaka huku mbunge akikosa kulikemea suala hilo na kuwa hivi sasa ameileta kamati hiyo kwa lengo la kuwarubuni.   

Sophia Mwaipyana mkazi wa kijiji cha Ikolo alikozaliwa Mbunge huyo aliuliza kuwa wakati akiomba kura aliahidi kuleta viwanda vya kusindika mpunga, Juisi, maji, afya, elimu, kujenga benki ya vikoba, kufufua vyama vya ushirika, kuleta Meli kwenye bandari ya Itungi kusomesha watoto yatima na wao kumuamini na kumpa kura za ndiyo.   

Alisema alipolitwaa jimbo hilo aliwageuka na kuamia Jijini Dar es Salaam akifanya kazi za Bandarini na kujiita mbunge wa Taifa bila kujali kuwa waliompa cheo ni wananchi wa Kyela na kibaya zaidi alisema alipolitwaa jimbo hilo hajawahi kuitisha mikutano ya wananchi na hata kuwashukuru.   

‘’Kamati hii ya miundombinu ameileta yeye ili apate kujisafisha na kutengeneza mazingira mazuri ya kutaka kugombea tena mwaka 2015 bila kujua kuwa sisi hatumtaki tena, wala Chama Chake kwa kuwa kuendelea kuwa na Ccm ni kuzidi kujiongezea mzigo wa matatizo’’alisema Mwaipyana.   

Dr, Mwakyembe anayejulikana kuwa mbunge machachari alishindwa kujibu mwaswali hayo zaidi alisema atampa siku tano mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Clement Kasongo ili ajibie,na kupelekea wananchi kuanza kumzomea na kutaka kumfanyia fujo ambapo aliokolewa na Prof,Kapuya kwa kujibu maswali.  

 Prof.Kapuya katika msafara huo uliozuiliwa na wananchi aliwaeleza kuwa malalamiko ya wananchi yapo sahihi na kuwa majibu ya nini kifanyike kuhusu marabara hiyo atayatoa baada ya siku saba na kuwataka wananchi wapishe msafara uendelee,na wananchi kutii ombi hilo.   

Gabriel Kipija Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa upande wake alisema wananchi wapo sahihi kuikata barabara hiyo kwani imekuwa ikijengwa chini ya kiwango na kubomolewa na kuwekwa viraka,na kuwa wizara ya Ujenzi chini ya John Magufuri kuiangalia kwa jicho la tatu barabara hiyo. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo