Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikua amepanga chumba cha
kuishi,Ruben Mollel alisema msichana huyo alikua anajulikana kwa jina la
Dada Pendo na kwamba maisha yake hayakua wazi.
“Alipokuja kupanga hapa alidai yeye ni mwanafunzi,ila hivi karibuni
alionekana kuwa mjamzito,hakuna kilichojulikana tena hadi jana ambapo
nyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitoto
kilichadhaniwa kuwa ni chake kikiwa kimezamishwa kichwa chini kwenye
ndoo ya maji”alisema baba huyo mwenye nyumba.
Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto huyo ndani ya nyumba ya dada
huyo ziliibuliwa na mpangaji mwenzake Mama Martha ambaye alidai kuwa
alisikia sauti ya mtoto akilia usiku kucha na baadaye kutoweka majira ya
asubuhi.
Baada ya juhudi za kuchunguza walikuta kichanga hicho cha kiume
kikiwa ndani ya ndoo na tayarikilikua kimefariki dunia huku mama yake
akiwa katika hali mbaya kutokana na kujizalisha mwenyewe.