Baada ya Ushindi wa Nani Mtani Jembe, matokeo ya mechi ya timu ya Simba
hayajawa mazuri siku za usoni, ni siku chache zimepita tangu timu hiyo
ipoteze mchezo wake wa nane katika mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania
bara.
Yanga iliamua kukatisha mkataba na Kocha Mbrazil, Marcio Maximo saa chache baada ya kushindwa katika mechi ya Mtani Jembe, taarifa ikufikie kwamba timu ya Simba imemfukuza kazi kocha wake mkuu Mzambia Patrick Phiri baada ya kuwa naye kwa muda wa miezi minne tangu alipojiunga na timu hiyo katikati ya mwezi wa saba.
Phiri amesimamishwa kazi baada ya mabosi wa Simba
kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo ambayo imefanya usajili mkubwa
wakati ligi iliposimama hali iliyopandisha matarajio ya mashabiki na
viongozi hali iliyobadilika wakati walipocheza mchezo wao dhidi ya
Kagera.
Kocha huyo amesimamishwa kazi pamoja na msaidizi wake wa kwanza ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye amekuwa na timu hiyo kwa muda mrefu tangu wakati wa Dravko Logarusic na kabla ya hapo alikuwa akiifundisha timu ya vijana.
Maamuzi hayo yalifanyika usiku wa jana
kuamkia leo kwenye kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya Double Tree
Masaki, Dar es Salaam ambapo viongozi wa juu wa klabu hiyo kwa kauli
moja walikubaliana kuwafukuza kazi makocha hao wawili.
Taarifa zilizopo chinichini ni kwamba nafasi ya Patrick Phiri itakwenda kwa kocha raia wa Serbia ambaye ni Goran Kapunovic huku msaidizi wake akitarajiwa kuwa kocha Mrwanda Jean Marie Ntagwabira.
Taarifa zaidi zinasema kuwa Suleiman Matola
ataendelea kuwa ndani ya klabu ya Simba ambapo atarudi kwenye nafasi
yake ya zamani kama kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka
20.