skip to main |
skip to sidebar
BASI LAPATA AJALI MLIMA KITONGA, NI BAADA YA KUANZA KURUDI KINYUMENYUME LENYEWE
Basi
liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa
likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.
Jitihada zikifanyika kulivuta basi hilo.
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia.
Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga baada ya kutumbukia.
Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine
yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo
cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye
uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili
kusubiri marekebisho hayo.
Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi,
likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu
aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.
(Habari/Picha: Global
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi