SERIKALI YATANGAZA KUJENGA BARABARA ZA KULIPIA

Screen Shot 2014-11-18 at 11.26.27 AMSerikali imetangaza rasmi kuanza mpango wa kutengeneza barabara zitakazotumiwa kwa kulipia kutoka Dar es salaam hadi Mkoani Morogoro.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja wakati foleni za barabarani zikizidi kuongezeka kwa kasi katika jiji la Dar es salam jambo ambalo limekua likilalamikiwa na wananchi.

Waziri wa Ujenzi John Magufuli alisema mradi huo utakua wa awamu mbili ambapo ya kwanza itaanza Dar hadi Chalinze na nyingine Chalinze hadi Morogoro.

Alisema sababu ya kuchukua uamuzi huo ambao umekua ukitumiwa na nchi nyingine zilizoendelea duniani imechangiwa na tathmini  iliyotolewa ikionyesha kwa siku zinapita  gari 56,000 katika barabara ya Morogoro.

“Kwa hali hii takwimu zinaonyesha  kati ya mwaka 2015 hadi2016 magari yatakuwa yakishikana kutokana na msongamano,ndipo tukafikiria utaratibu huu ambao utasaidia watu mbalimbali wenye uwezo wa kulipia ili wasikae katika foleni,”alisema Magufuli.

Alisema faida zitokanazo na utumiaji wa njia hizo utasaidia kuokoa muda na kupunguza ajali barabarani na gharama kidogo za mafuta kutokana na kuwa na mwendo kasi wa kilomita 120 kwa saa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo