Mwanamke Afanyiwa Ukatili wa Kutisha Jijini Arusha




Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Olkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amefanyiwa ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na kuondolewa kiganja cha Mkono, sikio na sehemu nyingine za mwili wake 
 
Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Paulina Joseph amefanyiwa ukatili huo na mtu anayedaiwa kuwa ni shemeji yake kwa madai ya kuingilia ndoa yake.
 
Tukio hilo lilimkuta bi Paulina akiwa shambani kwake akikata nyasi kwa ajili ya kulisha mifugo.
 
Mume wa Paulina ameeleza masikitiko yake kwa uongozi wa kijiji,Kitongoji na kata kwa kushindwa kumkamata mtuhumiwa na kutoroka kwani kitendo hicho kinaweza kusababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatii dhidi ta wanawake nchini.
 
Viongozi wa kijiji hicho wamekanusha kuwa hakuna uzembe uliofanyika kumkamata mtuhumiwa huyo kwani bado inaendelea kumtafuta  ili  kumtia hatiani.
 
Bi Paulina anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital Teule ya Seriani wilayani Arumeru alipolazwa na hali yake bado sio nzuri.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo