Habari za uhakika kutoka ndani ya kituo hicho zinasema baada ya
polisi hao kubaini kuwa mtoto huyo amefariki dunia waliamua kumuachia
mama huyo na maiti ya mtoto huyo kisha kutokomea kusikojulikana.
Baba mkubwa wa marehemu Shedrack Mwangu alisema polisi hao walifika
nyumbani kwa mdogo wake majira ya saa2 usiku na kumkamata shemeji yake
kwa madai ya kugombana na jirani yake.
Alisema hatua hiyo inatokana na shemeji yake huyo kumdai jirani yake
fedha za upatu anayejulikana kwa jina la Mama Na ambaye alikua
akimsumbua na kumdanganya wanachama wenzake bado hawajawasilisha.
Alisema shemeji yake alinyimwa dhamana na ndipo baba wa mtoto
alipowaomba askari hao kumchukua mtoto kutokana na hali yake kudhorota
ili wakampe dawa lakini walimkatalia na ilipofika alfajiri wakamtaka
mama huyo kuondoka kwa madai wao wanakwenda katika kazi zao huku tayari
mtoto huyo akiwa amefariki dunia.