Wanafunzi 387 wa vijiji vya kata ya nambisi wilayani mbulu mkoani manyara wanaosoma katika shule ya sekondari ya kata ya Murray wamelazimika kuacha masomo baada ya kushindwa kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 30 wa kwenda na kurudi kila siku kutokana na wanachi wa vijiji hivyo kuibua mgogoro wa kutaka kila kijiji kujenga shule yake.
Makamu mkuu wa shule hiyo Bw.Denis Lohay amesema baada ya wananchi
wa vijiji vya amoa,hhayloto na kwermusl kuigomea serikali akiwemo mkuu
wa wilaya hiyo kuwataka kujenga shule ya sekondari ya kata mpya katika
kijiji cha hhayloto baada ya kuanzishwa kwa kata mpya ya nambisi mvutano
huo pia umechangia msongamano huku wasichana 10 wakipata mimba katika
kipindi cha mwaka jana.
Kufuatia kuwepo kwa mvutano huo uliosababisha kila kijiji kuanza
ujenzi wake kwa madai kamati ya kata kutowashirikisha wananchi wa
vijiji hivyo na kuibuka kwa mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu sasa kila
kijiji kikiamua mipango yake baadhi ya wananchi wa vijiji cha amoa na
kwermusl wamemueleza mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Zacharia Isaay
hawatabadili uamuzi huo kutokana na uwezo waliokuwa nao.
Nae mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM
wilayani humo Bw.Zacharia Isay amesema serikali imetoa kibali cha ujenzi
wa shule ya kata ya hhayloto sanjari na maabara,lakini pia akalazimika
kuvunja mzizi wa fitna kuruhusu ujenzi wa shule katika kijiji cha amoa
mara baada ya wananchi hao kugoma kuchangia na kudai watajenga shule yao
bila ya msaada wa serikali.