kuhusu Mbunge David Kafulila
kufunga Ndoa Kigoma, JANA Novemba 24 kaingia ndani ya Jengo la Bunge
Dodoma na kupigiwa shangwe za mapokezi na Wabunge wa Bunge hilo wakati
kikao kikiwa kinaendelea.
Spika wa Bunge Anne Makinda alikuwa kwa kwanza kuzungumza wakati Wabunge wakimpigia makofi David Kafulila alipokuwa anaingia; “…
Bwana Harusi anaingia… Sasa Bibi Harusi yuko wapi mimi nilitegemea
anakuwa pale… Mchezo mbaya huo.. Haya asante nashukuru, hongera…“- Anne Makinda.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba naye aliongea haya; “… Na mimi napenda kuchukua fursa ya kumpongeza Mheshimiwa David Kafulila kwa kuoa, karibu kwenye klabu yetu na hongera sana… “
Bonyeza play hapa kusikiliza shangwe za mapokezi hayo Bungeni.