Mwanadada mwenye taito ya utangazaji na uigizaji wa sinema za
Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefungua kinywa na kutoa
la moyoni akisimulia tukio baya lililowahi kumkuta la jinsi alivyobakwa.
Akizungumza na Gpl, Aunty Lulu asiyeishiwa na vimbwanga alisema
kwamba, kamwe hawezi kusahau tukio hilo maishani mwake.
Aunty Lulu
aliyeng’ara kwenye Sinema ya Lost Soul alieleza namna alivyobakwa na
rafiki wa shemeji yake (rafiki wa mume wa dada yake) na kumpotezea ndoto
zake za kuanza mchezo huo akiwa ndani ya ndoa.
Akieleza kwa uchungu na masikitiko, Aunty Lulu alitiririka kwamba,
alikuwa akiishi kwa dada yake ambapo rafiki wa mume wa dada yake huyo
alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani kila wakati alipokuwa akifanya kazi
maeneo ya Posta jijini Dar.
Aunt Lulu alisema kwamba wakati
huo, yeye alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Kisutu, Dar, hivyo kila
siku jioni mwanaume huyo alikuwa akimpitia na kumpa lifti hadi
nyumbani.
Aliendelea kusema kwamba, siku moja jamaa huyo aliyekuwa
amemzidi umri maradufu alimtaka wafanye mapenzi lakini alimkatalia kwa
madai kwamba hakuwahi kufanya mchezo huo mbaya ambao alifundishwa kuwa
ni dhambi.
“Kwa kawaida yule jamaa alikuwa
akinifikisha nyumbani kwa dada yangu pale Makumbusho (Dar), ananisubiri,
nabadilisha nguo, naenda naye kwake maeneo ya Block 41 (Kinondoni)
ambako alikuwa akinifundisha. So alinibakia nyumbani kwake,” alisema
Aunty Lulu, mtangazaji wa zamani wa ITV na C2C.
Staa huyo aliendelea kutiririka
kwamba alipomwambia kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho, mwanaume huyo
alimwambia haamini ndipo akamkamata kinguvu na kumpeleka chumbani kwake
kisha akamwingilia na kumsababishia maumivu makali.
“Kwa kuwa niliumia sana, nilikuwa natembea kwa shida hivyo dada yangu aligundua.
“Kwa kuwa niliumia sana, nilikuwa natembea kwa shida hivyo dada yangu aligundua.
“Ilibidi dada anibane
kujua nina tatizo gani. Kwa kuwa nilikuwa sina ujanja nilimwambia
nimeingiliwa kwa mara ya kwanza lakini nilisita kumtaja mwanaume huyo.
“Dada aliponibana sana nilimwambia kwamba niliingiliwa na huyo rafiki wa mume wake.
“Lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana na ukweli liliwaumiza sana dada na shemeji yangu.
“Walimsema sana mwanaume huyo na ikawa ndiyo mwisho wa urafiki wao.
“Umri sikumbuki lakini
nakumbuka nilikuwa nakaribia kuingia kidato cha nne. Yule mwanaume
alizoea kuninunulia vifaa vya shule na kunisisitiza kusoma.
“Nilimuona mtu bora sana, nikamzoea na ikawa rahisi kwenda kwake
kusoma maana jamaa alikuwa ‘jiniazi’ na mwanzoni alikuwa jirani yetu
kabla ya kuhama.
“Ukweli huwa sipendi kuelezea historia ya maisha yangu ya mapenzi kwani inaniumiza sana.
“Huwa najisikia kulia
kwa sababu huyo rafiki wa shemeji yangu alinipotezea ndoto nilizokuwa
nazo kwamba nitafanya juu chini niolewe nikiwa ‘mbichi’ hivyo mapenzi
ningefanya nikiwa ndani ya ndoa.
“Sikufurahia kabisa kitendo hicho maana naona pia kiliniathiri kisaikolojia,” alisema Aunty Lulu.
“Baada ya tukio lile
aliomba anioe ili nimsamehe lakini nilikataa. Baadaye alikwenda kusoma
nje ndipo tukapotezana na sijawahi kumuona tena, nasimulia ili liwe
fundisho kwa wanawake wanaopenda kuwa na ukaribu kupitiliza na wanaume
wasiowajua kiundani,” aliweka nukta Aunty Lulu.