Wananchi wenye hasira kali wamewaua na kuwachoma moto watu wawili
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Tukio hilo limetokea leo tarehe
08/10/2014 saa 4:00 Asubuhi katika kitongoji cha NAMANDUNGUTUNGU,
maarufu kama MANZESE, kijiji cha SOMANGA, Wilaya ya kilwa Mkoa wa Lindi.
Watu hao wameuawa ikiwa ni siku
moja tu tangu Alipotekwa, kupigwa na kuuawa Mwendesha pikipiki mmoja,
maarufu kama bodaboda aliyeulikana kwa Jina la SELEMANI POMBE Mkazi wa
Kijiji cha Somanga siku ya Tarehe 06/10/2014 saa mbilin usiku.
Mwendsha
bodaboda huyo alipigwa na kuuawa kisha kunyang`anywa pikpiki yake aina
ya SUNLG yenye Namba za usajili T678 CYB.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Mitondo kijiji cha Somanga simu.
Mwendesha pikipiki huyo alitekwa na kuuawa alipokuwa anampeleka abiria
wake katika kitongoji cha Mitondo na inasemekana abiria huyo alikwenda
kukagua mkaa wake. Abiria huyo alifanikiwa kuwatoroka Majambazi hao
baada ya kufanikiwa kufungua kamba alizokuwa amefungwa mikononi na
miguuni baada ya kumjeruhi vibaya na kumbaka.
Watuhumiwa hao wa ujambazi wanasadikiwa kuwa ndio wanaofanya uhalifu katika maeneo ya
NYAMWAGE-MUHORO-MARENDEGO-SOMANGA, maarufu kama Eneo la Vumbi. Wanateka
magari,na kujeruhi watu, kulawiti na kuwanyang`anya fedha na mali
zingine kama simu, computer n.k
Mwandishi wa Habari hizi
amefanikiwa kupata jina la mmoja aliyeuawa kuwa ni RAMADHANI MAKUNGWA
mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa kijiji cha Somanga, na mwingine
hatujuweza kupata jina lake lakini kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya
raia zinasema mtu huyo ni Mwenyeji wa Lindi lakini yupo katika eneo hilo
kwa Muda mrefu kidogo.
Kuuawa kwa watu hao kumetokana Na msako
mkali ulioendeshwa na wananchi baada ya kukithiri kwa matukio ya
ujambazi katika maeneo ya kilwa kama Nangurukuru,
Miteja,Kipatimu,Njinjo,na somanga.
Kwani Mnamo tarehe 03/10/2014 majira
ya saa 4:30 usiku, gari zaidi ya kumi zilitekwa na Abiria, madereva na
mautingo kuporwa mali na fedha pamoja na baadhi yao kubakwa na
kulawitiwa na wengine kujeruhiwa Vibaya.
Tukio hilo la kusikitisha na
kuhuzunisha limetokea katika kijiji cha SNZA-MITEJA.
Baada ya
kuwakamata watu hao kabla ya kuwaua, mmoja alisema wasimuue ataonesha ni
wapi wenzao watatu walipo pamoja na pikipiki lakini kutokana na hasira za wanachi waliwaua na wengine wamezagaa katika pori la MIBUYU SABA
raia aliyetoa taarifa za kuonekana kwa watu hao na kufanikiwa
kuwakamata hao wawili aliwaona watu hao.
Hivyo Mpaka wakati huu
msako unaendelea, Wananchi wengi wamezagaa na kuzingira pori lote la
MIBUYU SABA kuwasaka hao watatu waliosalia pamoja na pikipiki
zilizoporwa.
MOTO UUONAO HAPO KWENYE PICHA HAPO CHINI NI HAO MAJAMBAZI WAKICHOMWA BAADA YA KUUAWA
CREDITS; RAMADHANI CHILEMBA