SERIKALI imefuta mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kuanzia mwaka huu ili kuboresha kiwango cha elimu nchini.
Tamko
hilo limetolewa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dkt.Shukuru Kawambwa wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu
Tabora, kilichoko Manispaa ya Tabora.
Alisema
kuanzia mwaka huu, Serikali imeyafuta mafunzo hayo ikiwa ni mkakati
maalumu wa kuboresha kiwango cha elimu ambapo walimu ambao wataajiriwa
kufundisha shule za msingi na sekondari, watatakiwa kuwa na elimu ya
kiwango cha diploma na kuendelea.
Aliongeza
kuwa, kuanzia sasa Wizara yake inataka kusimamia ubora wa elimu na
walimu ambao kuanzia mwaka huu, wale ambao wataajiriwa kufundisha katika
shule za msingi na sekondari, lazima wawe na elimu ya kiwango cha
diploma na wasiofikia kiwango hicho, watapewa fursa ya kujiendeleza bila
tatizo.
"Walimu
wa shule za msingi na sekondari na wahitimu wa kidato cha sita
waliopata daraja la 1-3 na kuchaguliwa kujiunga na kozi maalumu ya
ualimu ngazi ya cheti, watapelekwa vyuoni kupata masomo ya diploma
katika vyuo maalumu vilivyoandaliwa.
"Ili
kuhakikisha mpango huu unatekelezwa, Wizara inaandaa waraka maalumu wa
maelekezo ambao utatumwa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini,"
alisema Dkt. Kawambwa.
Awali,
akijibu swali la mwanafunzi wa chuo hicho aliyetaka kujua kwanini muda
wakufanya mazoezi kwa vitendo (BTP) umepunguzwa na kuwa wiki tatu badala
ya siku 60, Dkt. Kawambwa alisema utaratibu huo ni wadharura kutokana
na uhaba wa fedha.
Alisema
Serikali itajitahidi kurekebisha hali hiyo kadri hali ya kifedha
itakavyoruhusu ambapo akizungumzia ombi la kuongezwa posho kutoka sh.
4,500 wanazolipwa sasa hadi sh.7,500 ambazo wanalipwa wanafunzi wa ngazi
ya Shahada, aliahidi kulifanyia kazi suala hilo katika Bajeti ya
Wizara.
"Nawaomba
wanafunzi wote wa vyuo vya ualimu, kuhakikisha mnafaulu masomo yote
mnayofundishwa chuoni ili muweze kuajiriwa serikalini vinginevyo mtakaa
benchi," alisema.
Dkt.Kawambwa
alisema wakati anaingia katika Wizara hiyo, alisema hataajiri walimu
waliofeli, hivyo ataendelea na msimamo huo kwa nia njema, hivyo
wanafunzi waliopo shuleni wanapaswa kufaulu masomo yao na ya ziada ili
waweze kuajiriwa.