RAIA WA KIGENI WAKUTWA WAMEKUFA KWENYE CHUMBA KIMOJA HOTELINI JIJINI DAR




WATU sita wameaga dunia jijini Dar es Salaam wakiwemo raia wawili wa kigeni ambao wamekutwa wamekufa chumbani kwao na miili yao ikiwa haina jeraha lolote.
 
Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi, raia wa Afrika ya Kusini, Roxxane Hillier (27), aliyekuwa Meneja wa Mgahawa uitwao Water Front katika Hoteli ya Slipway Masaki na rafiki yake wa kiume aitwaye Hylton William aliyekuwa fundi wa boti maeneo ya Slipway walikutwa wamekufa wakiwa katika chumba chao walichokuwa wamepanga katika Hoteli ya Slipway.
 
Inadaiwa kwamba Hillier hakuonekana kazini kwa muda wa siku mbili na mara ya mwisho kuonekana ilikuwa Oktoba 12 mwaka huu saa 4.00 ambapo Oktoba 13 alitakiwa kuwa mapumziko na alitakiwa kazini Oktoba 14 lakini hakuonekana.
 
Inasemekana juhudi za kumtafuta zilianza kufanyika ambapo simu zake za mkononi zilipopigwa ziliita bila majibu na ndipo ufuatiliaji ulifanyika hadi mahali alipokuwa akiishi ambapo alikutwa yeye pamoja na mwenzake wakiwa wamefariki dunia ndani ya chumba chao cha kulala huku miili yao ikiwa haina jeraha lolote.
 
Katika eneo la tukio kulikutwa madawa mbalimbali ya usingizi aina ya Dayaspem, dawa za hospitali, Panadol, vichungi vya sigara, sigara aina ya Cornel yenye unga unga unaodhaniwa ni dawa za kulevya, chupa ya maji aina ya Kilimanjaro yenye maji ndani yake, chupa ya bia aina ya Castlelite ikiwa nusu na unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vifo hivyo huenda vimesababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi na matumizi ya dawa za kulevya. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo