RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya
Uteuzi wa Makadhi wa Wilaya za Unguja na Pemba.
Kwa mujibu
wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu
Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Makadhi hao ni Sheikh Ali Haruna
Ramadhan-Unguja na Sheikh Abubakar Ali Mohamed-Unguja.
Wengine ni
Mohamed Ramadhan Khamis-Unguja na Sheikh Omar Juma Othman-Pemba. Rais Shein
amefanya Uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 5 cha
Sheria ya Mhakama ya Kadhi Namba 3 ya mwaka 1985 kama ilivyorekebishwa na
Sheria namba 4 ya mwaka 2003.
Uteuzi huo
umeanza Septemba 12,2014