RAIS KIKWETE AWAPA URAIA WAKIMBIZI WA BURUNDI 162,156 MJINI TABORA


 Rais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora jana. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote kwani wakikiuka masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.  
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972. Tukio la utoaji wa vyeti hivyo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora mjini humo jana. Raia Kikwete katika hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.  
 Msoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao. Rais Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. 
Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo.  Picha zote na Felix Mwagara, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo