Katika
hali ya kustajaabisha kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la
Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la
Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji
huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso
Mara
baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na
kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo
haikujulikana maramoja imeandikwa nini
tukio hilo limetokea jana Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo,
katika
uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea jana usiku kwani
kutwa nzima ya jana hapakuonekana mtu ambae amekufa
mmoja
wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofisi
moja jirani na eneo la tukio( jina kapuni) amesema hii imekuwa ni mara ya
pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa ameuawa na kutupwa katika
korongo hili,hivyo anaviomba vyombo vya usalama kuweka doria ya mara
kwa mara eneo hili kwani eneo hili linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi
za Hazina Ndogo.
Polisi wakichukua vielelezo katika picha
Kutokana
na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya kumtoa
walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa gari la
'emegency' la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari mwili
kupandishwa juu kupelekwa eneo husika.
polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Mwili ukitolewa tayari kupelekwa kwenye gari la Polisi
Mwili ukiingizwa kwenye gari la Polisi kuelekea 'Central Police' kwa taratibu zingine