PICHA NYINGINE ZA AJALI YA LORI LA MAFUTA LILILOWAKA MOTO MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 6 wako katika hali mbaya kati ya majeruhi 17 wa ajali ya moto uliosabishwa na watu waliokuwa wakiiba mafuta baada lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta ya Petroli kuanguka karibu na makazi ya watu eneo  Mbagala charambe jiji Dar es salaam.

Mwandishi wetu amefika katika eneo hilo na kushuhudia mabaki ya lori lililokuwa limebeba mafuta ya Petroli huku maduka yaliyokuwa yamezunguka nyumba ya kulala wageni yakiwa yameteketea kwa moto wa Petroli uliosababishwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiiba mafuta bada ya lori HILO lililobeba mafuta kuanguka usiku wa kuamkia leo,ambapo inadaiwa miongoni mwa waathirika hao alichomoa Betri ya lori hilo na kusababisha mlipuko wa mafuta.
 
Kutokana na moto huo baadhi ya wafanyabiashara waliopoteza mali zao ambapo wengine mpaka sasa hawajajua thamani ya mali zililotekea ambapo mmoja wa wafayabiashara Bwana Ali Mohamed mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi amedai kupoteza malizenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 70, huku wengine wakitaka bima ya lori itumike kufidia mali zilizopotea. 
 
Akielezea tukio lilivyotokea mmoja wa wagonjwa Bwana Rajabu Selemani amesema baadhi ya watu walioungua akiwemo yeye alikuwa anapita barabarani akitokea kazini ndipo alipokuta barabara imetapakaa mafuta ya petroli na baadae moto mkali ghafla ukaanza kuwaka na kuwaunguza miguuni.
 
Muuguzi wa zamu wa hospitali ya temeke, Bi Rolesta Kinonda amesema hospitali wamepokea maiti 1 ya mwanaume, majeruhi 20, 19 wanaume na mwanamke ambapo kati ya majeruhi hao wanne wamewabakiza hospitali hapo na mwanamke ameruhusiwa baada ya kupata huduma ya kwanza.
 
Akizungumizia tukio hilo baada ya kutembelea wagonjwa katika hosptali ya taifa ya muhimbili na hospitali ya temeke, mkuu wa mkoa wa dar es salaam Bwana Said Mecky Sadiki amewataka wananchi wasilikimbile kuiba mafuta wakati malori ya mafuta yanapoanguka.
 
credits:itv


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo