Huku gharama ya ardhi ikizidi
kupanda, baadhi ya maeneo yaliosahaulika kama vile vyoo vya zamani
yamegeuzwa na kufanywa kuwa migahawa na maduka ya kuuza nguo.
Vyoo
vingi vya kukojoa vilisahaulika kwa miongo kadhaa baada ya vita vya
dunia vya pili ,lakini kufuatia hatua ya maafisa wa jiji hilo la kutaka
kupata mapato, mabadaliko hayo yanafanyika kwa kasi.
Baadhi ya
migawaha hiyo ni 'The Convinience' uliofunguliwa katika eneo la Hackney
mwaka 2013, 'WC' ambalo ni duka la mvinyo lililopo katika eneo la
Clapham kusini mwa London na 'ArtsLav' ambalo ni eneo la maonyesho
lililopo katika eneo la Kennington.
Kulingana na mtandao wa gazeti
la daily Nation nchini Kenya, Maeneo mengine yaliokuwa vyoo na kugeuzwa
ni 'the Attendant' na 'the Cellar Door' cabaret lililopo katikati ya mji
wa London.
Mwenendo huo ulianza hivi majuzi kulingana na Rachel
Erickson ambaye kazi yake ni kupanga mipango ya watalii kuzuru katika
vyoo hivyo hatua iliomsababisha kuitwa 'Mwanamke wa vyoo'.
Jayke
Mangio mwenye umri wa miaka 34,ambaye alifungua 'WC' mnamo mwezi
July,amesema kuwa serikali imekuwa ikilishinikiza baraza la jiji kutumia
maeneo yote yalio wazi kuleta mapato.
Baadhi ya maeneo ambayo yamevutia wawekezaji ni vyoo hivyo vya zamani na barabara za chini za treni.