Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema hatua ya
viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
kuingia katika makubaliano ya kushirikiana “ni kaburi la vyama hivyo.”
Wakati Nape akisema hayo, baadhi ya wasomi
wamesema ni hatua kubwa lakini yenye kuhitaji kuwa na sera na itikadi ya
pamoja.
Akizungumza kwa simu jana, Nape alisema Ukawa ni kaburi la vyama vya upinzani vilivyoungana kwa kuwa vitapoteza utambulisho wao.
Akizungumza kwa simu jana, Nape alisema Ukawa ni kaburi la vyama vya upinzani vilivyoungana kwa kuwa vitapoteza utambulisho wao.
“Huu ni mwanzo wa kumomonyoka kwa vyama vya
upinzani, moja vyama hivyo vitapoteza identity (utambulisho) zao na kama
mkutano wenyewe ndiyo umehudhuriwa na watu kidogo vile, basi hali yao
ni ngumu sana,” alisema Nape.
Alisema kutakuwa na mgogoro mkubwa hasa kwenye
nafasi za kugombea kwa kuwa hasa katika majimbo akitolea mfano wa Jimbo
la Ubungo ambalo alisema Julius Mtatiro wa CUF anataka kugombea huku
John Mnyika wa Chadema naye akitaka kutetea nafasi yake.
“Ukawa ni bomu ambalo litawalipukia na kwangu sijaona jambo jema kwa ushirikiano huo,” alisema Nape.
Hata hivyo, Nape alisema jambo moja ambalo vyama
hivyo vimelifanya ni kuunganisha nguvu kupambana na CCM ambayo misuli
yake ni mikubwa.
Na Boniface Meena, Mwananchi