Mwanamke mmoja amefariki wakati akifanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile.
Mwanamke huyo raia wa Uingereza mwenye
umri wa miaka 24 amefariki nchini Thailand alikokwenda kufanyiwa
upasuaji huo, ambapo taarifa kutoka nchini humo zinasema baada ya
kupatiwa vidonge vya usingizi mapigo yake ya moyo yalisimama.
Taarifa kutoka Thailand zinasema
upasuaji huo ni wa awamu ya pili kufanyiwa, baada ya kutoridhiwa na
matokeo ya upasuaji wa awali.
Waziri wa afya Boonruang Triruangworawat amesema jitihada zilizofanywa kuokoa maisha ya msichana huyo hazikusaidia.
Daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji
huo aliyefahamika kwa jina la Dk. Sompob Sansiri anashikiliwa na polisi,
huku serikali ikitangaza kuifungia kliniki alipokuwa akifanyia upasuaji
kwa siku 60 kwa ajili ya kupisha uchunguzi.
Inasemekana kuwa unafuu wa huduma hiyo
unapelekea watu wengi kutoka nchi za Ulaya kukimbilia Thailand licha ya
kuripotiwa kutokea vifo vingi vya wateja wake.