MWANAMUME mwenye umri wa miaka 30 amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa baada ya kumuua mkewe kwa kumchinja shingo kwa kisu kutokana na kile alichodai kuwa ni kudharauliwa na mkewe.
Tukio
hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, Geofrey
Kamwela ambaye amemtaja mwanamume huyo kuwa ni Ramadhani Abdallah,
mkulima na mkazi wa kijiji cha Makale katika kata ya Mitundu, tarafa ya
Itigi wilayani Manyoni anayedaiwa kumuua mkewe, Amina Waziri (30).
Katika
tukio hilo la Oktoba 20 saa 9.15 alasiri, Kamanda Kamwela alidai kuwa
Ramadhani baada ya kuhakikisha kuwa mke wake amekufa, alichukua kamba ya
katani na kujitundika kwenye moja ya kenchi ya nyumba yao na kujinyonga
hadi kufa.
“Kabla
ya kujinyonga, Ramadhani aliacha ujumbe mfupi usemao kuwa amechukua
hatua hiyo ya kukatisha maisha yake na mke wake kutokana na mkewe huyo
kushirikiana na kaka zake kumuoza binti yake wa kufikia bila ridhaa
yake,” alisema Kamanda Kamwela.