MKE AMDHALILISHA MUMEWE KWENYE TV, ASEMA INGEKUWA AMRI YAKE ANGEOMBA UUME WAKE UBADILISHWE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHz74_QDLnK_LpMKI2_6pNhZUbnt5M3e2nWizGeRZHfSXxtFCuxnmQzEKaA3nsmSS8ZYBdnur6PlXYZws1od6oskK-onh4PfGpGTJtDBC7YlmvdvQkJrMMnKMmOumy6WLTbQugBEUHwpeL/s1600/1.jpgKuna mchezo wa Television (TV game show) unaoitwa “Family Feud,” ambao unashindanisha familia mbili. Familia inayopata points nyingi zaidi, kutokana na majibu yao, inashinda na kupata zawadi. 

Sasa huyu mama, mume wake akiwa pembeni kama mshiriki mwenzie, aliulizwa. “Kama ungekuwa na uwezo wa kubadilisha sehemu moja tu, ya mwili wa mumeo, ungebadilisha sehemu ipi?” Mwanamke huyo akajibu “penis” au “uume.” 

Kwa kuwa ni kawaida kwa wanawake wa USA kusema wanapenda mwanaume awe na uume mkubwa, na hulalamika kwa rafiki zao wakikutana na mwanaume mwenye “kiduchu,” kauli ya mama huyu ilichukuliwa kumaanisha kuwa mumewe ana “kiduchu;” kitu kilichomuacha host Steve Harvey na wahudhuriaji wamepigwa na butwaa. Walishangazwa na jibu hilo huku wakionekana kujiuliza, mke huyo anaweza vipi kumdhalilisha mumewe mbele ya taifa zima; huku mumewe akionyesha kushikwa na aibu huku akijikaza kisugusugu.

Baadhi walimtetea mama huyo wakisema hakujibu kutokana na ukubwa wa nyeti za mumewe, bali alitaja jibu alilodhani litakuwa na points nyingi zaidi. Points zinatokana na jibu la mshiriki kufanana na jibu lililojibiwa na wanawake 100 walioulizwa swali hilohilo. 

Mfano kama wanawake 20 kati ya 100, walitoa jibu linalofanana na lako, unapata points 20, kama mmoja kati ya 100, unapata point moja. Kwa hili, huyu mama aliambulia patupu maana katika wanawake 100 walioulizwa swali hilo, hakuna aliyetaja kutaka kubadilisha uume wa mumewe.

Lakini wabishi wamekataa utetezi huo. Wanasema kwamba kwa mwanamke huyo kufikiria hivyo kwa haraka haraka, sababu hakujua kama ataulizwa swali hilo kabla, inaonyesha ana tatizo na nyeti za mumewe. 

Na kwamba wanawake wengine 100 walioulizwa kwa siri hawakutoa jibu hilo ni ushaidi zaidi kwamba jibu la mama huyo halihusiani na kupata points nyingi, bali alitoa lake la moyoni. Baadhi ya wanaume wanasema wangempa talaka mara moja.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo