MGOGORO WA MAITI WAINGIA SIKU YA 43 LEO, MAITI YAENDELEA KUSOTA MOCHWARI

Mgogoro wa kifamilia kuhusu mwenye haki ya kuzika mwili wa Rosemary Marandu (38), umeingia siku ya 43 leo, huku ukiendelea kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
 
Mwili wa marehemu huyo aliyefariki dunia Septemba 4, mwaka huu umehifadhiwa hospitalini hapo na unalipiwa Sh9,000 kwa siku, gharama ambayo hadi leo imefika Sh387,000.
Akizungumza jana, baba wa marehemu, Flavian Marandu, alitoa ruksa ya kuzikwa mwili huo, huku akijiweka kando akidai hana mamlaka ya kuzika mke wa mtu.
Wiki moja iliyopita, mume wa marehemu, Sigfrid Mlingi alimtuhumu baba mkwe wake huyo kuzuia mwili huo na baadaye kumtolea lugha chafu.
“Mimi ndiye nilimuuguza Hospitali ya Mawenzi hadi kunifia mikononi, nilipokwenda Keryo na kuonana na baba mkwe, akanifukuza,” alidai Mlingi.
Mlingi alisema awali walikubaliana kumzika Septemba 9 katika Makaburi ya Karanga, Manispaa ya Moshi lakini baadaye mkwewe alikataa.
Lakini jana, Marandu alisema: “Huyo ni mke wa mtu...kama kuna mtu ana shida akachukue kibali akazike, mimi sina kibali,” alisema.
Marandu alisema tangu msiba huo utokee, ametuma marafiki zake kuzungumza na ndugu ili mazishi hayo yafanyike baada ya kuridhiwa na mume na mama mzazi lakini hawatoi ushirikiano.
Lakini ndugu mwingine wa marehemu, Bertha Akwilin alipoulizwa jana, alikiri kuzungumza na Marandu juzi na kumwelekeza kwenda kuchukua kibali kutoka kwa mtu aitwaye Tesha.
“Ni kweli nimepata bahati ya kuzungumza na baba (Marandu) na akatoa ruksa hiyo lakini mama wa marehemu na wana ndugu bado wanatafakari ukweli wa kauli ya Marandu,” alisema.

Na Daniel Mjema, Moshi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo