MASIKINI....MWALIMU AGONGWA NA DALADALA NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO


MWALIMU mmoja mkazi wa Mlole Manisapaa ya Kigoma Ujiji amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace yenye namba CMS 688 inayofanya safari zake Kigoma mjini kwenda Kijiji cha Simbo wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa, Kamishna Msaidizi (ACP), Michael Deleli, alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 2:00 asubuhi na kumtaja aliyefariki kuwa ni Godness Masuruli (30), aliyekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari hilo lililokuwa likiendeshwa na John Makosa (34).

Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake huku dereva akiwa mahabusu na atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo