MAAJABU; MTI ULIODONDOKA MIAKA 3 ILIYOPITA WAINUKA NA KUSIMAMA WIMA KAMA ZAMANI HUKO TABORA



Wananchi wa kijiji cha Mfuto katika Kata ya Ufulumo huko Wilayani Uyui, Tabora wamepatwa na mshituko na kuingiwa na hofu baada ya mti aina ya msufi, uliong'oka na kuanguka miaka mitatu iliyopita, kuinuka na kusimama wima kama zamani. 
 
Mti huo wenye kipeo cha futi mbili inaelezwa kuwa ulianguka kwa upepo mkali na kuungua kwa moto wakati wa kuandaa mashamba. Mtangazaji wa TBC anasema kuwa mti huo ambao ulikuwa umeshambuliwa na mchwa, hivi majuzi ulionekana ukinyanyuka taratibu kana kwamba walikuwepo watu wanaunyanyua hadi uliposimama kama awali.
 
Mara baada ya kuenea kwa taarifa za kuinuka kwa mti huo, wananchi wengi walifika kwenye eneo husika na kuanza kugombea vipande vya mti huo, ambapo kila mtu alitaka kupata walao gome au sehemu yoyote ya mti huo ama hata udongo palipokuwa pamelala mti huo.
 
Afisa Mtendaji wa Kijii hicho, amesema kuwa Serikali ya Kijiji inaendelea kuwasiliana na Wazee wa kimila ili kupata maoni yao juu ya tukio hilo.

Tazama  Video  hapo  chini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo