Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akionesha kadi 27 za wananchama wa Chadema
waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM kaatika mkutano wa hadhara
uliofanyika Mjini Nyololo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama
na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010. Kulia aliyevaa
shati jeupe ni aliyekuwa Katibu wa Kata ya Igowole, Josephat Soda ambapo
wengine ni miongoni mwa walio kuwa wafuasi wa Chadema.
Aliyekuwa Katibu wa Chadema
Kata ya Igowole, Joephat Soda akikabidhi bendera ya chama hicho kwa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya yeye na wenzie 26
kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Kinana akimkabidhi kadi ya CCM, Josephat Soda baada ya kutanga kujiunga na CCM katika mkutano huo.
Josephat Soda akielezea jinsi
alivyoamua kuondoka Chadema na kujiunga na CCM, ambapo alisema amechoka
na chama kilichosheheni uongo, ambapo viongozi wa Chadema alidai kuwa
walitoa maagizo kuwaakope fedha za kujengea Mnara wa mwandishi wa
habari Marehemu David Mwangosi, aliyeuawa wakati wa vurugu za Chadema na
Polisi katika Mji wa Nyololo, ambapo walimuahidi kumtumia fedha
zilizotumika kujenga mnara huo ahadi ambayo hadi sasa haalipwa na
anadaiwa na muuza simenti na muuza saruji alikokopa. CCM imeamua kulipa
madeni yote aliyokuwa akidaiwa.
Wanachama wa CCM wakiwemo wapya kutoka Chadema, wakiapa kiapo cha utii cha CCM baada ya kukabidhiwa kadi wakati wa mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA )