JESHI LA POLISI LIMESITISHA MAFUNZO KWA ASKARI 132 HUKO ZANZIBAR, KISA AFYA ZAO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9Z5OmP8hgUoLpzP5hqVyJW1tkOcrXeKhIi7PhzlIOMJSotO87Ysc_JZwWvU7ZsKRPTJaBngbSYzB0gKkYsYuGSNnPkYHjDkyL3tKO93aCcV0aTlS2MGXtHnt_ehGADAU6GJJfhQJrgnFk/s1600/F.jpgJeshi la polisi limesitisha mafunzo kwa askari132 waliokua katika chuo cha Polisi Zanzibar kwa kile kinachodaiwa kuwa ni sababu za kiafya.

Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari chuoni hapo kati ya askari hao walioondolewa chuoni hapo mwishoni mwa juma lililopita mmoja wao Koplo Abdalah alifariki dunia akiwa chumbani kutokana na shinikizo la damu baada ya kupata taarifa ya kuondolewa chuoni.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Makame alisema amewasitishia kufanya mafunzo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya lakini ajira zao zitaendelea kama kawaida na wataendelea na kazi zao.

Alisema askari aliyefariki alikua akisumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu na alifariki wakati wenzake wakijiandaa kwa mazoezi ya asubui chuoni hapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo