Afisa elimu katika kaunti ya Bungoma
Kenya, ametoa taarifa kuhusiana na wanafunzi 53 wanaofanya mitihani wa
kumaliza elimu ya sekondari iliyoanza siku ya Jumanne wiki hii, ni
wajawazito.
taarifa iliyochapishwa na news 24 Kenya
imesema Charles Anyika; mkurugenzi wa elimu wa kaunti hiyo amesema
idadi hiyo imebainika baada ya kufanya uchunguzi, na kuongeza kuwa
anategemea idadi ya wanafunzi wenye ujauzito ni kubwa kuliko
iliyopatikana kwa kuwa baadhi ya wakuu wa shule walitoa taarifa za uongo
na pia baadhi ya familia wamekuwa ‘wakimalizana’ na watuhumiwa bila ya
kutoa taarifa.
Amesema awali kabla ya uchunguzi huo
walitegemea idadi ya wanafunzi wenye mimba kufikia 100, wakati huo huo
amewataka walimu wawaache wanafunzi hao wafanye mitihani yao kwa utulivu
na kuwaagiza walimu kuandaa magari ambayo yatasaidia iwapo mwanafunzi
yoyote atapata dharura.
Anyika amewataja walimu, waendesha
‘bodaboda’, na wanaume waliooa ni wahusika wa mimba hizo na kuongeza
kuwa umaskini ni chanzo kikubwa cha tatizo hilo, na kuwataka wazazi
kuwalinda watoto wao na kuwapa elimu juu ya hatari ya mimba za utotoni
pamoja na ngono zembe.