Waombolezaji wakilia kwa unchungu kanisani.Kwa mujibu wa
vyanzo vya habari, mwanamke huyo ambaye mumewe ni kigogo mwenye cheo cha
mkurugenzi wa kampuni moja ya usafirishaji jijini Dar, alikutwa na mauti baada
ya kuingia kwenye gesti hiyo na mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa ni hawara yake
licha ya kuwa na mume.
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo, Nickson John alisema siku
ya tukio, mwanamke huyo na jamaa yake aliyevaa kofia maarufu kwa jina la
kapelo, walifika kwenye gesti hiyo saa saba mchana.
Alisema: “Waliulizia chumba chao cha siku zote maana walikuwa
wakifika kila wakati, nikawaambia kiko wazi.
Ndugu na jamaa wa karibu wakiomboleza msibani.“Nilifuatana
na mwanaume hadi kwenye chumba hicho namba 5, alilipia kisha kuzama na huyo
mwanamke.“Saa kumi mwanaume alitoka,
akaniambia anakwenda kutafuta chakula endapo mwanamke wake atahitaji kinywaji nimpe.
“Ilipofika saa kumi na mbili jioni, nilianza kuingiwa na
hofu kwani yule mwanaume alikuwa hajarudi na mwanamke hakutoka kuhitaji
kinywaji.“Niliamua kwenda kugonga mlango lakini hakuitika. Niliendelea kukaa
kusubiri kama yule mwanaume atarudi lakini wapi!
Padri akiweka msalaba juu ya kaburi la marehemu Juliet
Gayton Komba.“Saa moja usiku nikiwa sijawaona, nikaenda kugonga kwa nguvu huku
nikiita bila mafanikio, bosi wangu aliyelala chumba kingine alinisikia
akaja.“Nilimweleza tatizo naye aligonga hakuna aliyeitika, tukazunguka
dirishani kuchungulia, tukamwona mwanamke amelala kitandani lakini tulipata
wasiwasi huenda alipatwa na tatizo.“Bosi wangu aliwapigia simu polisi, walifika
na kuvunja mlango ambapo walimkuta mwanamke amekufa huku akitokwa damu mdomoni,
waliuchukua mwili hadi Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa uchunguzi.”
Kwa upande wake, Deusi Komba ambaye ni mume wa marehemu
alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri kutokea.Alisema asubuhi ya siku hiyo
alimuacha marehemu nyumbani na kwamba hakuwa na mpango wa kutoka lakini
aliporudi jioni hakumkuta na simu yake kila alipoipiga ilikuwa ikiita bila
kupokelewa.
Juliet Gaison Komba (37) .Alisema ilibidi aende Kituo cha
Polisi Maturubai kutoa taarifa na ndipo alipoelezwa kuwa, mkewe huyo anayemsaka
amekutwa amekufa gesti.Marehemu huyo alizikwa Jumanne iliyopita katika Makaburi
ya Mbagala Kuu, Dar na ameacha watoto watatu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,
(pichani) alipoulizwa alikiri kutokea kwa tukio na kusema uchunguzi unaendelea.