GADNER G HABASH AITOSA TIMES FM, SASA KUHAMIA REDIO EFM

Imepita takriban miaka miwili tu baada ya kuingia mkataba na Times 100.5 FM, mtangazaji maarufu nchini Gardner Habash sasa yupo mbioni kuacha kazi katika kituo hicho. 

Habari za uhakakika ambazo hazina shaka zinapasha kuwa mtangazaji huyo ataanza kazi mpya na kituo cha EFM 93.7 pia cha jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Taarifa News, Habash amesema ameangalia maslahi na nia yake ni kutanua mawazo na mbinu za utangazaji kwa vile amepewa fursa pia ya kuwa mwandaaji wa matamasha. 

Vituo vyote viwili viko maeneo ya Kawe jijini Dar Es Salaam na unaweza kusema ni majirani kwa kiasi fulani. 

EFM licha ya upya wake imepata umaarufu wa aina yake kutokana na style mpya waliyokuja nayo, wengi wanashabikia sana vibwagizo vya Mkude Simba…!!! Video ya Gardner akiongelea swala hilo hii hapa.credits:taarifa news


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo