CHID BENZI KUPANDISHWA KIZIMBANI KESHO KWA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

MSANII wa muziki wa hip hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za kulevya na kesho anatarajiwa kufikishwa mahakamani. 

Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya juzi jioni katika Uwanja wa Kimataifa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam wakatia wa ukaguzi kabla ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Alfred Nzowa, msanii huyo ameendelea kushikiliwa na jeshi la polisi mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani.

Alisema Chidi Benz alikamatwa na dawa aina ya Heroine kete 14 na misokoto miwili ya bangi, vyote alikuwa ameiweka katika mfuko wa shati alilokuwa amevaa.

“Dawa alizokamatwa nazo zilikuwa kwa ajili ya matumizi yake, jeshi limeendelea kumshikiria mpaka Jumatatu kwa sababu leo (jana) na kesho (leo) sio siku za kazi,” alisema.

Mbali ya dawa, msanii huyo alikutwa katika begi yake na kigae kidogo cha chungu na kijiko, ikiwa ni maandalizi ya kutumia dawa hizo.

Msanii huyo alikuwa anakwenda jijini Mbeya kwa shoo ya ‘Instagram Party’ iliyofanyika jana katika ukumbi wa City Pub, jijini humo.

Chidi Benzi alikuwa ameongozana na msanii mwenzake Nurdin Bilal ‘Shetta’ ambaye naye alishikiliwa kwa muda kabla ya kuachiliwa kuendelea na safari yake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo