BOKO HARAM KUWAACHILIA HURU WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOWATEKA

Serikali ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.

Mkuu wa jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.

Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.

Kulingana na afisa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad Idris Derby.

Alisema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.

Pia alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau.

>>>BBC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo