BASI LA GRAZIA LAPATA AJALI NA KUUA ABIRIA MKOANI MOROGORO


Ajali mbaya ya basi la kampuni ya Kwa Wapendwa (GRAZIA) lenye namba za usajili T 951 BBK kutoka mkoni Njombe kwenda Dar es Salaam yaua mmoja huku abiria zaidi ya 50 wakinusurika.

Ajali hiyo imetokea Leo Majira ya saa 6 mchana katika barabara kuu ya Iringa -Dar es Salam kwenye kijiji  cha Msimba  mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Mmoja Kati ya abiria wa basi hilo John Sanga ameueleza mtandao huu kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kuendesha kwa Mwendo kasi katika eneo hilo lenye kona kali kabla ya kuligonga lori lililokuwa limesimama mbele yake.

Sanga alisema kuwa dereva huyo alilazimika kuingia katika lori hilo kukwepa kugongana uso kwa uso na lori  lililokuwa mbele yake kutoka Morogoro.

"Dereva wetu alikuwa katika Mwendo Mkali sana kwani iwapo angekuwa katika Mwendo wa kawaida baada ya kuliona lori hilo mbele na hakuna uwezekano wa kupita angeweza kusimama"

Hata hivyo alisema kutokana na ajali hiyo mmoja Kati ya abiria aliyekuwa amekaa siti ya mbele kushoto kwa dereva ndie aliyepoteza maisha eneo la tukio na baadhi ya abiria kupata majeraha ya kawaida na kukimbizwa hospitali .

Mmoja Kati ya askari waliokuwepo eneo la tukio ambae hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro alidai kuwa ni mtu mmoja pekee ambae ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na miaka Kati ya 50 na 55 ndiye aliyefariki na jina lake halijaweza fahamika.

Aidha alisema chanzo ni dereva wa basi hilo la abiria kulazimisha kupita pasipo na njia huku akijua wazi lori la mbele yake lilikuwa limesimama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro hakuweza kupatikana kuelezea zaidi tukio hilo mpaka tunakwenda mtamboni.  

chanzo: www.matukiodaima.co.tz


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo