Wazazi wa mtoto Mazoea mkazi wa Rufiji wanashikiliwa na Polisi kwa
tuhuma za kumtupa mtoto huyo kwenye jiko lenye moto wakimtuhumu kuiba
shilingi 6000 za jirani yao, Kamanda wa Polisi alisema wazazi hao
wanashikiliwa kwa kosa hilo na watapandishwa kizimbani leo kujibu
tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa ofisa Mtendaji wa kijiji cha Kilimani alisema
watuhumiwa hao walifanya kosa hilo baada ya mmoja wa majirani zao kudai
ameibiwa kiasi hicho cha fedha ambapo baba yake alimshika miguu na mama
yake mikono kisha wakamtupa ndani ya jiko na kuungua vibaya mkono wa
kulia wakidai wanamwadhibu kutokana na tabia yake mbaya.