Kufuatia
tukio la Msanii wa muziki Chidi Beenz kukamatwa na dawa za kulevya
katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Kamanda wa
Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aonya vijana
kutokujihusha na dawa hizi kabisa.
Kamanda
Nzowa amesema kuwa tukio la kukamatwa kwa msanii huyu mkubwa, ni nafasi
ya jamii na vijana kujifunza na kuachana na dawa hizi ambazo madhara
yake kwa jamii ni makubwa.
Chidi baada ya upekuzi alipatikana na kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi, tukio ambalo limeendelea kuzua maoni tofauti kutoka kwa watu mtandaoni wakati huu ambapo anasubiri hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.

Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa