YANGA YAICHAPA AZAM 3-0, YATWAA NGAO YA JAMII



KIKOSI cha Yanga SC kimetwaa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa timu ya Azam FC mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Geilson Santos 'Jaja' dakika ya 56 na 66 huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Simon Msuva dakika ya 87 ya mchezo.

Hii ni mara ya pili Yanga kuifunga Azam katika mechi za Ngao ya Jamii baada ya msimu uliopita watoto wa Jangwani kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa Salum Telela "Essien".


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo