Wajumbe waliotembelea hifadhi ya taifa ya Kitulo wakiongozwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wameonesha kuguswa na kituo cha watoto yatima Fema Matamba na kuamua kuchanga fedha kwa ajili ya Kituo hicho.
Wajumbe hao walichanga fedha zao kwa hiari ambapo walikabidhi kiasi cha tsh 138,000/= taslimu ambazo walizikabidhi kwa mlezi wa kituo hicho.
Hatua hiyo inatokana na kituo hicho kinacholelea watoto yatima kuhitaji misaada kwa kuwa bado hakijaweza kuwa na miradi inayokiingizia kipato kiasi cha kuweza kulea watoto hao bila msaada wa watu mbalimbali.
Fedha hizo zilikabidhiwa na afisa maliasili na mazingira Bw Uhuru Mwembe kwa niaba ya mkuu wa wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Makete.
Mlezi wa kituo hicho aliwashukuru kwa msaada huo na kusema kuwa wameonesha moyo wa kipekee na watalipwa na mwenyezi Mungu kwa kuwa ni jukumu la kila mmoja kusaidia watoto yatima kwa kadri atakavyojaliwa na mwenyezi Mungu
Na Eddy Blog, Makete