AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka.
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri
alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo
chanzo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo
ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi,
sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati
mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa
sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa,
ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea
na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida
sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya
Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya
kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya
kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi
kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho
na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri
kwenye kampuni yake.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema
anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja
na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta
fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia
mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa
likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu
ambalo ni Toyota Harrier.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya
kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku
tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila
kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa
sharti la kutoanika jina , rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa
staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi
zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa
watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama
ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye
wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya
mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo
wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo
zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na
Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo
sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza
akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume,
jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu
la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji
Diamond mtandaoni.
Chanzo: Ijumaa wikienda/gpl
Chanzo: Ijumaa wikienda/gpl
