Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo walivamia
katika kituo kikuu cha polisi Wilaya ya Bukombe Mkoani saa 9 alfajiri
wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurusha kwa mkono.
Mwandishi Victor Bariety anasema kwa mujibu wa taarifa
alizozipata ni kwamba majambazi hao walizingira kituo hicho hadi eneo la
mapokezi(CRO)na kuanza kuwamiminia risasi za moto askari waliokuwa
zamu.
Kufuatia hali hiyo askari wawili kati ya wanne waliokuwa kituoni hapo
walipoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za
miili yao.
Akiongea
na blog hii mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe Dkt Honorata
Rutatinisibwa amekiri kupokea miili ya askari wawili wa kike na
kiume ambao ni WP 7106 PC Uria Mwandiga na askari namba G.2615 Pc
Dustani Kimati.
Askari
waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwenye namba E.5831
CPL David Ngupama Mwalugelwa aliyejeruhiwa kichwani na usoni na kwamba
ameumizwa vibaya sehemu za midomo yake huku meno mawili yaking'oka na Mohamed Hassani Kilomo ambye amejeruhiwa kifuani na mguu wa kulia uliovunjika mfupa kwa kupigwa risasi.
Kwa mjibu wa Dr Honoratha kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya
wamewapa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa
tukio na kuahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Na Victor Bariety-Geita