KAULI ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ya kuagiza yafanyike maandamano na migomo nchi nzima bila kikomo, ikiwezekana hata bila ya kibali cha Polisi, imelichefua Jeshi la Polisi.
Jeshi hilo limeonya kuwa halitasita kumchukulia hatua kali, kwa kuwa anavuka mipaka ya kisiasa na kugeukia makosa ya jinai.
Aidha,
limemtaka kuacha mara moja kuihamasisha jamii, kutofuata sheria na
taratibu za nchi, kwani nao atakuwa anawaingiza matatani.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi ilitolewa jana na Kamishna wa Jeshi hilo anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi ilitolewa jana na Kamishna wa Jeshi hilo anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Alisema
endapo Mbowe na wafuasi wake, watafanya migomo na maandamano bila ya
kufuata sheria, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake, kwa kuwa tayari
alishapewa onyo mara ya kwanza kufuatia kauli hiyo.
Alisema
Mbowe anatakiwa kufuata taratibu na sheria kuhusu kufanya maandamano,
kwani taratibu zote zipo, hivyo kwa kauli zake hizo, anavunja sheria na
kuvuka mipaka iliyowekwa kugeuka kuwa jinai na siyo siasa.
‘’Kauli
iliyotolewa na Mbowe Septemba 14 (juzi) inaashiria uvunjifu wa amani na
inahamasisha jamii kutotii sheria na taratibu za nchi. Tunaonya kwamba
Mbowe anatakiwa kufuta kauli yake na kwamba taratibu zote zilizowekwa
zifuatwe,’’ alisema Chagonja.
Awali,
alisema kwamba siasa zina mipaka yake, hivyo mtu atakayetumia mwavuli
wa siasa kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo, jeshi hilo
halitamvumilia na halitasita kumchukulia hatua kali kama mhalifu
mwingine.
‘’Masuala
ya Bunge yana sheria na taratibu zake, hivyo kuna masuala mengine ya
ndani ambayo hayatakiwi kutolewa nje bila ya kufuata taratibu
zilizowekwa na bunge hilo, haikumpasa kusema kwamba atashinikiza wafuasi
wake na wananchi kufanya maandamano yasiyofuata sheria,’’ aliongeza.
Aidha,
aliwaonya wananchi wote kuzingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa
katika kutekeleza jambo lolote, pia kuepuka kauli zitakazowashawishi
kuvunja sheria hizo.
Alisisitiza
kuwa ili kuimarisha amani na utulivu uliopo, wananchi wanatakiwa
kutoshiriki katika masuala ya uvunjifu wa amani kwa namna yoyote, badala
yake kushiriki katika shughuli zao za kulijenga taifa na kuleta
maendeleo.
Wabunge wacharuka
Wakati Jeshi la Polisi likionya kuhusu kauli zinazotajwa kuwa za kichochezi za Mbowe, Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba nao jana waliibuka na kulishutumu kundi la wajumbe wa bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuhamasisha watu kuandamana barabarani, kupinga kuwepo kwa Bunge hilo huku viongozi wa kundi hilo wakionesha kuwa mstari wa mbele.
Wakati Jeshi la Polisi likionya kuhusu kauli zinazotajwa kuwa za kichochezi za Mbowe, Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba nao jana waliibuka na kulishutumu kundi la wajumbe wa bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuhamasisha watu kuandamana barabarani, kupinga kuwepo kwa Bunge hilo huku viongozi wa kundi hilo wakionesha kuwa mstari wa mbele.
Wajumbe
hao pia wameshutumu kitendo cha Ukawa, kumwandama Mwenyekiti wa Bunge
hilo, Samuel Sitta kwa kufafanua kwamba Bunge hilo, sio mali ya Sitta,
bali linafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye ameshutumiwa
kuwa ndiye chanzo cha vurugu na chokochoko, zinazoendelea kufanywa na
UKAWA, kutokana na kauli zake, ambazo amekuwa akizitoa kuwa Bunge hilo
limepoteza uhalali wa kisiasa.
Akizungumza
wakati wa majadiliano bungeni, George Simbachawene alisema Ukawa
wamekuwa wanafanya upotoshaji mkubwa kwa kuutangazia umma kuwa uwepo wa
bunge hilo sio halali. Alionya kuwa wananchi sasa wanapaswa kupima
uzalendo wa viongozi wa kundi hilo kupitia kauli zao.
Alisema
Bunge hilo, sio mali ya Sitta ambaye ni Mwenyekiti na kuwa kiongozi
huyo na hata Rais, hana mamlaka ya kulisitisha, kwani linaendeshwa kwa
mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Alisema kwa wingi wa wajumbe walioko bungeni, hawawezi kuwa wendawazimu kuendelea na jambo ambalo sio halali.
Alisema
kuwa wale ambao waliamua kutoka nje ya Bunge hilo, ndio ambao wamevunja
sheria. Simbachawene alisisitiza kuwa wanachofanya wajumbe hao ni
kupinga Katiba inayopendekezwa.
Alihoji; “Hivi
kuingia barabarani kuandamana ndio kutunga Katiba ya wananchi? Halafu
hao Ukawa ndio wanataka tuwape nchi, kwa kweli naomba wananchi wawaone
kwamba watu hawa ni wabaya”.
Aliwahadharisha
wananchi wasiende kuandamana, badala yake wasubiri wapige kura ya
kuikubali au kuikataa Katiba hiyo na sio kwenda kuandamana.
Simbachawene
ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, alikiri kuwa bunge hilo limewakosa walio nje kwa
sababu waliwahitaji ili wachangie mawazo mbadala, lakini wamekosa
uzalendo kwa kukataa kurejea bungeni.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya
aliwashangaa Ukawa kuwachochea vijana waandamane nchi nzima wakati
viongozi wao hawashiriki maandamano hayo.
Alisema
Chadema na washirika wake wa Ukawa, wasiwapeleke vijana ambao ni
tumaini la taifa hili kwenye maandamano, kwani kufanya hivyo ni hatari
kwa maisha ya vijana hao ambao ni nguvukazi ya taifa.
Kapteni
John Komba, yeye katika mchango wake alitumia muda wake mwingi,
kumshutumu Jaji Warioba, kuwa ndiye aliyesababisha vurugu zote
zinazoendelea nchini juu ya mchakato wa Katiba.
Alisema
Jaji Warioba aliheshimiwa na Rais Jakaya Kikwete na wananchi
walimheshimu, ndio maana alikabidhiwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa
ajili ya kukusanya na kuandika mabadiliko ya Katiba na wakati huo
Watanzania walikuwa kimya.
Alisema
yeye baada ya kumaliza kazi yake, kazi hiyo sasa ni ya Bunge Maalumu la
Katiba, lakini kila kinachofanywa na bunge hilo Jaji Warioba anawakosoa
na alimwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo, atoe tamko la kumkemea
mwanasheria huyo.
Komba
ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, alishauri Jaji Warioba akae
kimya katika kipindi hiki ambacho bunge hilo linamalizia kazi yake ya
kuandika katiba hiyo.
Komba
pia alimshutumu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kujigeuza kuwa
Amiri Jeshi kwa kutangaza vita na kuwataka wafuasi wake waingie
barabarani nchi nzima katika maandamano ambayo hayana kikomo.
“Si
mlimsikia akisema ‘mko tayari kwa vita?’ Wakamjibu ‘tuko
tayari’…akaendelea, ‘lakini mjue kuna risasi mko tayari’ na wafuasi wake
wakajibu ‘ndio tuko tayari’… hivi hii ni amani gani wanayoitangaza huko
nje, hii ni hatari kwa nchi,” alisema Komba.
Amos
Makalla, mjumbe na Mbunge wa Mvomero ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Maji, aliungana na wajumbe wengine, kuwashambulia Ukawa bungeni. Alisema
kuwa umoja wao huo, maana yake ni umoja wa katiba ya wachache na sio ya
wananchi, kama wanavyojitangaza.
Alisema
kama ingekuwa ni umoja wa katiba ya wananchi walio wengi, kundi hilo
lingebaki ndani ili waandike na kushiriki kwenye mambo yanayogusa
wananchi wao ;na sio kutoka nje ya Bunge.
Alimtaka Sitta asitishike na kauli za Ukawa, badala yake awe imara ili kazi iliyobaki ya kuandika Katiba ya nchi imalizike.
Mwenyekiti
wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa aliliambia bunge hilo kuwa wenzake hao
wa upinzani, wanamsakama Sitta kwa kuwa ndiye alikuwa chaguo lao wakati
wa mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa bunge hilo.
Alisema
wakati wa mchakato wa kumchagua mwenyekiti, vyama vyote vya upinzani
venye wabunge ambavyo vinaunda Ukawa, walimuunga mkono Sitta kwa
mategemeo kuwa angelinda maslahi yao.
Mwanasiasa
huyo ambaye mara nyingi amekuwa anatofautiana na misimamo ya Ukawa
tangu bunge hilo kuanza, alisema waliamini kuwa Sitta angewaunga mkono
katika hoja zao za ovyo, ambazo alidai hazina faida kwa nchi, ndio maana
wanamshambulia kila kukicha.
Mohammed
Misanga alimtaka Sitta asitetereke kwa kuitwa king’ang’anizi, kwani
wananchi walio wengi wanaliunga mkono bunge hilo, kutokana na mambo
mengi yanayojadiliwa kuwahusu wao.
“Nimeongea
na wananchi kwenye jimbo langu na kule Dar es Salaam wanawashangaa hawa
Ukawa, maana haya mambo tunayozungumzia hapa ni ya wananchi wenyewe,” alisema Misanga ambaye pia ni Mbunge wa Singida Magharibi.
