MOTO WATEKETEZA FAMILIA HUKO GEITA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watoto watatu wa familia moja wameteketea kwa moto hadi kuwa majivu huku mmoja akibaki kichwa tu baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuteketezwa kwa moto katika mtaa wa Nyankumbu mjini Geita.

Akisimulia mkasa huo Baba wa familia hiyo Robert Reginald amewataja watoto wake waliokufa kuwa ni Dimijius (4), Sofia (6), Reginald Robert (8) ambaye kichwa chake pekee ndicho kilichobaki huku wengine viugo vyao vikibaki kama mkaa.

Wathirika wengine ni mwanae Scholastika (16) ambaye yeye akipelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando alikokuwa amelazwa (ICU) na mkewe aliyemtaja kwa jina la Angelina Gasper yeye ameungua vibaya mkono wa kulia ambaye hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya.
FP_Moto_01
Haya ni mabaki ya vitu vilivyoungua ndani ya nyumba hiyo,wakiwemo kuku kama inavyoonekana katika picha
FP_Moto_04
Haya ndio makaburi matatu ambapo miili ya watoto watatu imezikwa
CHANZO:FIKRAPEVU


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo