AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BAISKELI KYELA-MBEYA

Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Lughano John aliye na miaka 36 mkazi wa Ipinda Juu ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya marehemu kutuhumiwa kuwa ameiba baiskeli.
 
Tukio hilo limetokea jana asubuhi ya saa nne katika kitongoji chaLutusyo, kijijini Talatala katika Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani hapa Mbeya.
 
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio zinaeleza kwamba marehemu Lughano John alikamatwa na wananchi hao akiwa na baiskeliya wizi na kisha kuanza kumshambulia kwa kumpiga hali iliyopelekea kifo chake. 
 
Wakati msako wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ukiendelea, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tikio hilo na  kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawe na tabia ya kuwapeleka watuhumiwa wanaokwamatwa katika mamlaka husika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo