Napenda kuwajulisha kwamba mtoto Faith amepatikana maeneo ya
Msasani na ameshaungana na familia. Aliokotwa na Msamaria mwema ambaye
nae alikuwa anafanya juhudi za kuitafuta familia yetu.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana sana kwa msaada wenu wa kurusha habari ile ya kupotea kwake. Lakini zaidi sana nawashukuru jinsi mlivyotenda kwa haraka (act promptly) nilipotuma tu ujumbe.
Hii imeonyesha umuhimu wa mitandao hii na ni kweli ya wananchi na jamii.
Asanteni sana na kila la heri.